1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Ushindani mkubwa kuliwakilisha eneo la Latina Amerika katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD25

Hadi sasa kiti cha muakilishi wa eneo la Latina Amerika katika Baraza la usalama la Umoja wa mataifa kimesalia tupu baada ya kutopatikana mshindi kati ya Guatemala na Venezuela zilizokuwa zikiwania nafasi hiyo. Baada ya raundi 10 za kura, hakuna aliyepata theluthi mbili za kura zinazohitajika. Kura imepangwa kupigwa tena leo. Kura hiyo imegeuka ushindani mkubwa kati ya Marekani na rais wa Venezuela Hugo Chavez, ambae amekuwa akijaribu kutafuta uungwaji mkono katika nchi za Ashia, Afrika na Mashariki ya kati ili kukabiliana na maslahi ya Marekani.