1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Umoja wa mataifa walaani shambulio dhidi ya jengo la bunge mjini Baghdad.

14 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCA5

Umoja wa mataifa umelaani shambulio la bomu la Alhamis nchini Iraq dhidi ya jengo la bunge na kutoa wito wa maridhiano kati ya makundi ya kidini nchini humo.

Jeshi la Marekani limesema majeshi ya usalama ya Iraq yana uwezo wa kulinda mali za serikali, licha ya shambulio la kujitoa muhanga , ambalo lilifanyika katika eneo ambalo lina ulinzi mkali mjini Baghdad la zoni ya kijani.

Luteni Jenerali Ray Odierno amewaambia waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka katika mji huo mkuu wa Iraq kuwa ana imani na uwezo wa Wairaq kuweza kulinda usalama.

Maafisa wa Marekani hivi sasa wanasema kuwa mlipuko huo katika jengo la mkahawa limeuwa mbunge mmoja na kuwajeruhi wengine zaidi ya 20. Ripoti za mwanzo zimesema kuwa watu wanane wameuwawa. Kundi la wapiganaji lililo na mahusiano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda limedai kuhusika na shambulio hilo.