1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Ugonjwa wa ukimwi wazidi kutapakaa

22 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqV

Ripoti ya Umoja wa mataifa inasema watu kiasi ya milioni 4,3 duniani waliambukizwa virusi vya ukimwi mwaka huu wa 2006 na kupandisha idadi ya watu wenye kuwa na virusi vya ukimwi kufikia milioni 40. Ripoti hiyo inasema virusi vya ukimwi vimezidi kuongezeka hasa kwa wanawake.

Kulingana na ripoti hiyo, mwaka huu idadi ya wanaoambukizwa virusi vya ukimwi iliongezeka katika maeneo ya Sovieti ya zamani, eneo la kusini na kusini mashariki mwa Asia kutokana hasa na matumizi ya madawa ya kulevya na vitendo vya zinaa bila kinga. Eneo la kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika linashikiria rikodi mbaya kuhusu ugonjwa wa ukimwi ambako watu walioambukizwa virusi vya ukimwi wanafikia karibu milioni 25, ikiwa na theluthi mbili za watu wanaotembea na virusi vya ukimwi duniani.

Habari njema ni kuwa utoaji madawa ya kupooza madhara ya ukimwi uliboreka mnamo miaka ya hivi karibuni.