1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Ripoti kuhusu mauaji ya Rafik al-Hariri

13 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjG

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaochunguza mauaji ya aliekeuwa waziri mkuu wa Lebanon,Rafik al-Hariri wamesema,wamewatambua watu fulani wanaoshukiwa kuhusika na mauaji hayo.Hariri aliuawa Februari 14 mwaka 2005,baada ya mshambuliaji aliejitolea muhanga kujiripua ndani ya gari katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Shambulizi hilo pia liliua watu wengine 22.