1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mswada wa kufungua mahakama kuhusu al-Hariri

18 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC13

Mswada wa azimio ukitoa mwito wa kuwa na mahakama ya kuwashtaki wale wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon,Rafik al-Hariri,umewasilishwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York. Uingereza,Ufaransa na Marekani zimependekeza mswada huo,kuambatana na ombi rasmi lililotolewa na waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora.Ombi hilo limetolewa na Siniora baada ya spika wa bunge la Lebanon Nabih Berri kukataa kuitisha kikao cha kuidhinisha hatua hiyo.Umoja wa Mataifa na serikali ya Lebanon tayari zimetia saini makubaliano ya kuwa na mahakama hiyo.