NEW YORK : Miaka sita ya mashambulizi ya Septemba 11 | Habari za Ulimwengu | DW | 11.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK : Miaka sita ya mashambulizi ya Septemba 11

Mji wa New York leo utabakia kimya kwa dakika nne kwa heshima ya kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 ambayo yameuwa takriban watu 3,000 miaka sita iliopita.

Kumbukubu kuu zitafanyika katika mtaa wa Lower Manhattan ambapo kwa mara ya kwanza zitakuwa hazifanyiki katika eneo hasa kulikotokea mashambulizi hayo ambapo kulikuwako majengo ya Vituo vya Bishara Duniani kutokana na ujenzi wa kumbukumbu unaofanyika kwenye eneo hilo hivi sasa.

Majina ya watu waliouwawa yatasomwa na kubakia kimya kwa muda wakati wa saa 8.46 saa za mji huo ambapo ulikuwa ni wakati hasa ndege ya kwanza ilipobamizwa katika jengo linajulikana kama Mnara wa Kaskazini.

Rais George W. Bush wa Marekani anatazamiwa kuhudhuria misa ya kumbukumbu mjini Washington.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com