1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Leo ni siku ya Ukimwi.

1 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnf

Siku ya ukimwi duniani inaadhimishwa duniani kote leo wakati ugonjwa huo ukiendelea kuleta maafa na watu wanaokadiriwa kufikia milioni nne wakiambukizwa virusi vya HIV kila mwaka.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan amewataka watu kuendelea na mapambano dhidi ya ukimwi, akiongeza kuwa wanasiasa wanapaswa kuwajibika.

Nae rais wa zamani wa Marekani ambaye mfuko wake wa kumabana na ugonjwa wa ukimwi unasaidia miradi kadha ya aina hiyo katika bara la Afrika leo amesema kuwa juhudi lazima zichukuliwe katika kuyasaidia makampuni ya madawa kupunguza gharama.

Katika sherehe za maadhimisho hayo mjini New York , Bwana Annan amesema kuwa virusi vya ukimwi ambavyo vimeuwa watu zaidi ya milioni 25 na kuambukiza watu milioni 40 zaidi, ni changamoto kubwa katika enzi hizi.