NEW YORK: Jopo la kimataifa lataka vikwazo dhidi ya serikali ya Sudan | Habari za Ulimwengu | DW | 12.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Jopo la kimataifa lataka vikwazo dhidi ya serikali ya Sudan

Jopo linashughulikia migogoro ya kimataifa limesema juhudi za kidiplomasia zimeshindwa kutatua mgogoro wa Darfur magharibi mwa Sudan ambapo watu zaidi ya laki mbili wameshauawa. Kinachohitajika sasa jopo hilo limeshauri ni vikwazo dhidi ya serikali ya Sudan ili kuweza kuepusha maafa zaidi kwa watu wa jimbo hilo.

Asasi hiyo imeitaka jumiya ya kimataifa isimame pamoja juu ya suala la Darfur la sivyo serikali ya Sudan itaendelea kunufaika na mgawanyiko wa jumuiya hiyo.

Wakati baadhi ya nchi kama Marekani na Uingereza zinatetea ulazima wa kupeleka jeshi la kimatiafa katika jimbo la Darfur, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Jan Pronk anatetea hoja ya kuliimarisha jeshi la Umoja wa Afrika ambalo sasa linalinda amani katika jimbo hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com