1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Jan Pronk atarudia Sudan

28 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyb

Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Sudan, Jan Pronk, ambae alifukuzwa na serikali ya Sudan, atarejea nchini Sudan na kuendelea na kazi zake hadi utakapomalizika muda wake nchini humo. Msemaji wa Umoja wa mataifa, Stephanne Dujarric, amesema katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Kofi Annan, amethibitisha kuwa Jan Pronk ndie ataendelea kuwa muakilishi wake nchini Sudan. Serikali ya Sudan ilimuambia Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan kwamba imempa Jan Pronk muda wa siku tatu awe ameondoka kutoka Sudan baada ya kuandika katika mtandao wake kwamba jeshi la serikali lilishindwa hivi karibuni katika mapigano mawili na waasi katika jimbo lenye machafuko la Darfur, magharibi mwa Sudan.