1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Hukumu ya kuwanyonga wasaidizi wa Saddam yapingwa na umoja wa mataifa.

16 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaB

Umoja wa mataifa umesema haukupendezwa na hatua ya serikali ya Iraq ya kuwanyonga wasaidizi wawili wa Saddam Hussein. Katibu mkuu Ban Ki-moon amesema kuwa Iraq imepuuzia miito ya umoja wa mataifa ya kutochukua hatua ya kuendea na hukumu ya kifo.

Mjini Rome, rais wa halmashauri ya umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso na waziri mkuu wa Italia Romano Prodi wameshutumu hatua hiyo ya kunyonga ambayo imetekelezwa mjini Baghdad mapema siku ya Jumatatu. Wakati wa utekelezaji wa hukumu hiyo ya kunyongwa, kichwa cha ndugu yake Saddam Hussein , Ibrahim al-Tikriti kilikatika kutoka katika mwili wake. Pamoja na Saddam , ambaye alinyongwa wiki mbili zilizopita , watu hao wawili waliopitishiwa hukumu yao, walihukumiwa kwa makosa dhidi ya ubinadamu.