NEW YORK: Deutsche Welle na Umoja wa Mataifa kushirikiana | Habari za Ulimwengu | DW | 07.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Deutsche Welle na Umoja wa Mataifa kushirikiana

Umoja wa Mataifa na Deutsche Welle zimetia saini makubaliano ya kushirikiana upande wa televisheni redio na mtandao wa Internet.Makubaliano hayo yametiwa saini na Mkurugenzi wa Deutsche Welle, Erik Bettermann na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Sashi Tharoor mjini New York.Kuambatana na makubaliano hayo,pande hizo mbili kila juma,pamoja zitatayarisha kipindi cha televisheni kuhusika na mada ya utandawazi.Na upande wa matangazo ya redio,Umoja wa Mataifa na Deutsche Welle zitabadilishana vipindi ambavyo hasa vitahusika na bara la Afrika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com