1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI:Kansela Angela Merkel anaendelea na ziara yake nchini India

30 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BI

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiendelea na ziara yake ya siku nne nchini India amezungumzia azma ya serikali yake ya kuimarisha na kuzidisha uhusiano katika sekta tafauti pamoja na India.

Bibi Merkel amesema India ni mshirika wa Ujerumani wa kimkakati.

Kansela Merkel na mwenyeji wake waziri mkuu wa India Manmohan Singh wameshuhudia uzinduzi wa safari ya treni ya kiufundi kwa jina Science Express iliyotengenezwa kwa ushirikiano wa pamoja na makampuni mashuhuri ya Ujerumani BASF na Bosch.

Treni hiyo itakuwa imeizunguuka miji 56 ya India hadi kufikia mwezi Juni mwakani.

Akizungumzia kuhusu ufundi wa hali ya juu wa treni hiyo kansela Angela Merkel amesema.

Baadae leo jioni kansela Merkel atakutana na waziri mkuu Manmohan Singh kwa mazungumzo ya kina pamoja na kutia saini makubaliano kadhaa katika sekta ya ushirikiano wa kisayansi, kijeshi na haki miliki.

Kesho kansela Angela Merkel anatazamiwa kwenda Mumbai ambako atahutubia baraza la ushirikiano wa kiuchumi la Ujerumani na India.