NEW DELHI:India yaadhimisha miaka 60 ya uhuru | Habari za Ulimwengu | DW | 15.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW DELHI:India yaadhimisha miaka 60 ya uhuru

India inasherehekea miaka 60 ya uhuru tangu kumalizika kwa utawala wa Uingereza nchini humo.Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh alihutubia taifa na kuwaeleza wananchi kuwa hatua zimepigwa ila mengi mazuri yako njiani.Ulinzi mkali uliwekwa kote nchini ili kuzuia uwezekano wa ghasia kuzuka hasa katika maeneo ya vita kama Kashmir.Huduma za simu za mkono zilisitishwa ili kuzuia ghasia kuzuka.Waziri Mkuu Manmohan Singh ameahidi msaada wa dola bilioni 6 ili kuimarisha sekta ya kilimo.Kwa mujibu wa kiongozi huyo kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa hilo. Rais wa India Pratibha Patil naye alisistiza umuhimu wa ujenzi wa taifa

''Maendeleo ya uchumi sharti yaimarishe maisha ya watu wa kawaida hususan wanaoishi katika umasikini.Kuna ushahidi kuwa wanawake wetu wanatimiza majukumu yao ya nyumbani aidha ujenzi wa taifa.''

Pakistan iliadhimisha miaka 60 kwa sala na kunyamaa kimya kwa dakika moja ili kuwakumbuka maelfu ya raia wake waliopoteza maisha yao mwaka 47.Malkia Elizabeth wa Uingereza na Waziri Mkuu Gordon Brown walituma pongezi zao kwa India na Pakistan na kuwatakia kila la kheri.

India ilipata uhuru wake Agosti 15 mwaka 47 wakati utawala wa koloni la Uingereza ulipomalizika.Hatua hiyo ilisababisha eneo hilo kugawanywa na kuwa India na Pakistan.,

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com