1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI : Mtu mmoja mbaroni kwa uripuaji wa treni

20 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQR

Polisi ya India inamhoji mwananchi wa Pakistan kuhusiana na kuhusika kwake na miripuko ya mabomu iliouwa takrriban watu 66 kwenye treni ya abiria ya India.

Polisi pia imetowa michoro ya watu wengine wawili inaoaminika kuwa waliruka kutoka kwenye treni hiyo inayojulikana kama Treni ya Urafiki kabla ya kuripuka kwa mabomu hayo.

Tukio hilo limelaaniwa vikali na Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh na Rais Pervez Musharaf wa Pakistan.

Wakati huo huo Waziri wa mambo ya nje wa Pakistan Khurshid Kasuri anatazamiwa kuwasili mjini New Delhi kwa ziara ya kiserikali nchini India.Kasuri ameahidi kuendelea na ziara hiyo yenye nia ya kuendeleza mchakato wa amani kati ya India na Pakistan licha ya uripuaji huo wa treni uliotokea Jumapili.