NEW DELHI: Mamilioni watengwa kwa mafuriko kusini mwa Asia | Habari za Ulimwengu | DW | 05.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW DELHI: Mamilioni watengwa kwa mafuriko kusini mwa Asia

Idadi ya watu waliopteza maisha na makazi katika mafuriko,kusini mwa bara la Asia,inatazamiwa kupanda juu.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa haya ni mafuriko mabaya kabisa kupata kushuhudiwa. Hadi hivi sasa,watu 249 wamefariki katika mafuriko yaliyosababishwa na msimu wa mvua kubwa. Kama watu wapatao milioni mbili,wametengwa kwa mafuriko nchini India,Bangladesh na Nepal.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com