1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NDJAMENA: Waasi wa Chad wapambana na vikosi vya serikali

Waasi mashariki mwa Chad,wameudhibiti mji mkuu wa eneo hilo,Abeche,baada ya kupigana vikali na vikosi vya serikali.Jeshi la serikali limesema limerudi nyuma ili kuzuia hasara ya maisha ya raia.Wanadiplomasia na mashirika yanayotoa misaada yameripoti juu ya uporaji katika mji wa Abeche ulio kilomita 160 kutoka mpaka wa Sudan.Mji huo ni kituo cha makundi mengi ya misaada yanayohudumia wakimbizi kutoka Chad na jimbo la magharibi la Sudan,Darfur.Serikali ya Chad inaituhumu Sudan kuwa inawasaidia waasi, lakini Khartoum inakanusha lawama hizo.Kwa upande wake Sudan,inaituhumu Chad kuwa inawasaidia waasi wenye asili ya Kiafrika katika jimbo la Darfur.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com