1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege za NATO zafanya mashambulio baada ya kuwa kimya kwa siku tatu

Abdu Said Mtullya15 Juni 2011

Baada ya kupumzika kwa siku kadhaa NATO imeanza tena kumshambulia Gaddafi

https://p.dw.com/p/11aMB

Ndege za kivita za NATO zimezishambulia tena sehemu kadhaa za mji mkuu wa Libya, Tripoli. Kwa mujibu wa taarifa za waandishi wa habari milipuko mikubwa miwili iliutikisa mji wa Tripoli.

Kabla ya mashambulio hayo kufanyika jana jioni, ndege za NATO zilitawanya vipeperushi katika mji wa Zlitan kuwataka wanajeshi wa Kanali Gaddafi wasalimu amri. Wapinzani wa Gaddafi wanaulenga mji huo uliopo umbali wa kilometa 160 mashariki ya Tripoli. Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba waasi wameshauteka mji wa Kikla magharibi mwa Libya.

Wakati huo huo jumuiya ya NATO imehakikisha kwamba inazo nyenzo za kutosha za kuiwezesha kuendelea na vita dhidi ya Kanali Gaddafi, licha wa wasi wasi uliopo kwamba ari ya jumuiya hiyo inadhoofika wakati Gaddafi anajiimarisha. Msemaji wa mfungamano huo wa kijeshi ameeleza mjini Brussels kwamba , NATO inazo nyenzo za kutosha.

Hapo awali maafisa wa ngazi za juu wa Ufaransa na Uingereza walionyesha wasi wasi juu ya muda unaochukua katika vita vya Libya

.