1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ndege za kivita za jeshi la Kenya zimeuwa wanamgambo 50 wa al Shabab

Ndege za kivita za Majeshi ya Kenya zimeshambulia kambi za wanamgambo wa al Shabab huko kusini mwa Somalia na kuwauwa takribani wanamgambo 50 na wengine 60 kujeruhiwa vibaya.

epa03025947 Somali security officers secure the scene of a suicide car bomb explosion as the burning car is seen at the KM4 junction in Mogadishu, Somalia, 06 December 2011. A witness said at least four people including a bomber were killed when the car was stopped by soldiers and a driver detonated the vehicle that was full of explosives. EPA/ELYAS AHMED +++(c) dpa - Bildfunk+++

Wapiganaji nchini Somalia

Msemaji wa Jeshi la nchi hiyo Meja Emmanuel Chirchir amesema kundi al Shabaab lenye mafungamano na kundi la kigaidi la al Qaeda ambalo kwa hivi sasa lipo upande wa kusini wa Gaebahare lilikuwa likipanga kuyashambulia majeshi ya Kenya na Somalia katika miji miwili ya karibu ambayo ilidhibitiwa na vikosi vya Kenya wiki hii.

Akizungumza na Shirika la Habari la Uingereza, Reuters, msemaji huyo aliongeza kusema shambulio hilo ni pigo kubwa kwa wapiganaji hao waliokuwa wakipanga kushambulia wanajeshi wa Kenya waliokuwepo katika miji ya Fafadun na Elade.

Kenya ilipelekea majeshi yake katika ardhi ya nchi jirani ya Somalia Oktoba mwaka jana baada ya kutokea matukio ya utekaji nyara na mashumbilo katika maeneo ya mipakani yaliyofanywa na kundi la al Shabaab ambayo yalitishia kuzorotesha sekta ya Utalii ya Kenya.

Kundi la al Shabaab limekuwa kitisho kikubwa cha usalama katika eneo la Afrika Mashariki, jambo lililoufanya Umoja wa Afrika wenye kikosi cha ulinzi wa amani huko katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, kutanua mamlaka ya ulinzi wa amani na kuomba Umoja wa Mataifa kuliongezea nguvu jeshi hilo kufikia wanajeshi 18,000.

Awali Kenya ilisema inadhibiti miji ya Fafadun na Elade iliyopo kusini magharibi mwa jimbo la Gedo, baada ya kutokea mapigano yaliyosababisha vifo vya wapiganaji watatu wa al Shabab.

Mwandishi: Sudi Mnette/RTR
Mhariri: Josephat Charo

 • Tarehe 07.01.2012
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13fjM
 • Tarehe 07.01.2012
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13fjM

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com