Ndege ya watalii ya One Two Go yadondoka Phuket | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 17.09.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Ndege ya watalii ya One Two Go yadondoka Phuket

Ndege moja ya abiria iliyokuwa ikisafirisha watalii imedondoka kisiwani Phuket ilipojaribu kutua kukiwa na hali mbaya ya anga.Yapata abiria 88 wamepoteza maisha yao huku wengine wakiteketea kwa moto na kujaribu kutorokea madirishani

mabaki ya ndege ya One Two Go iliyodondoka Phuket

mabaki ya ndege ya One Two Go iliyodondoka Phuket

Ndege hiyo ya tikiti za bei nafuu ya kampuni ya One Two Go ilikuwa na abiria 123 na wafanyikazi 7 waliotokea mjini Bangkok na kuelekea kisiwa cha Phuket kabla kuteleza kwa mujibu wa maafisa wa serikali.Ndege hiyo iligonga ukuta kabla kuvunjika vipande viwili.Kulingana na manusura moshi uligubika kila kitu huku miale ya moto ikiteketeza baadhi ya abiria wengine waliojaribu kutoroka kupitia madirishani.

Idadi kamili ya watalii wa kigeni bado haijulikani japo 78 waliokuwamo safarini walitokea mataifa ya Ufaransa,Ujerumani,Israel,Australia na Uingereza kwa mujibu wa naibu gavana wa jimbo la Phuket.Serikali imetoa orodha ya wataalii 30 wa kigeni walionusurika huku maiti 60 zikitolewa kwenye mabaki ya ndege hiyo.Shughuli ya kutoa miili iliyosalia ilichukua muda mrefu zaidi.

 • Tarehe 17.09.2007
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CB1D
 • Tarehe 17.09.2007
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CB1D

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com