1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege ya abiria yapata ajali Angola

20 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cuzl

LUANDA: Hakuna alienusurika katika ajali ya ndege ya abiria iliyotokea nchini Angola.Watu wote 12 waliokuwemo katika ndege hiyo wamepoteza maisha yao.Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, ndege hiyo iliripuka baada ya kugonga mlima katika hali mbaya ya hewa.