1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi masikini zatengewa dola millioni 500

11 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CaBB

BALI.Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na masuala ya hali hewa unaendelea huko Bali Indonesia umekubaliana kufadhili mfuko utakaosaidia nchi masikini kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mfuko huo mpya umepangwa kuanza mwaka 2012 ukiwa na dola millioni 500.

Fedha hizo zitatumika kujengea mabwawa au mifumo ya umwagiliaji mashamba katika nchi ambazo zimeathiriwa na hali ya ukame au kupanda kwa kina cha bahari.

Hata hivyo wakosoaji wamedai kuwa kiwango kilichotengwa kwa ajili ya mfuko huo hakitoshi kikifananishwa na kile kilichotengwa kwa ajili ya nchi zilizoendelea kukabiliana na mabadiliko ya hali hewa katika miongo ijayo.Kiwango hicho ni dola billioni 85 kwa mwaka.