1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nawaz Shariff arejea nyumbani kutoka uhamishoni Suudia

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSxK

Lahore(Pakistan):

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Shariff amerejea nyumbani hii leo baada ya kuishi miaka sabaa uhamishoni nchini Saud Arabia.Kabla ya kuondoka Madina,Nawaz Shariff alihimiza sheria ya hali ya hatari iliyotangazwa November tatu iliyopita ibatilishwe.Wakati huo huo Polisi wamewakamata maelfu ya wafuasi wa chama cha Muslim League ,kuwazuwia wasimpokee kwa shangwe waziri mkuu huyo wa zamani.Watu elfu tatu wamekamatwa leo asubuhi amesema msemaji wa chama cha Muslim League Ahsan Iqbal.Mamia ya polisi wametawanywa katika maeneo yanayopelekea uwanja wa ndege wa Lahore.Nawaz Shariff amerejea nyumbani kwa lengo la kupigania kiti uchaguzi mkuu utakapoitishwa Pakistan january nane ijayo.KIongozi mwengine wa upinzani Benazir Bhutto anasema ameshajaza hati za kupigania uchaguzi wa bunge wa huko Karachi .