1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yashambulia Tripoli

Halima Nyanza(ZPR)28 Mei 2011

Mashambulio mapya yaliyofanywa na jeshi la Jumuia ya Kujihami ya NATO jana usiku dhidi ya mji mkuu wa Libya Tripoli, yalilenga wilaya iliyo na makaazi ya kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.

https://p.dw.com/p/11PfL
Anga ya mji mkuu wa Libya Tripoli, baada ya mashambulio ya ndege za NATOPicha: dapd

Mripuko mkubwa uliitikisa wilaya ya Bab Al-Aziziya,  eneo lisilo mbali na katikati ya mji huo. Mripuko mwingine ulitokea dakika chache baadaye.

Huu ni usiku wa nne mfululizo, kwa eneo la mji huo kulengwa katika mashambulio katika ya anga.

NATO Luftangriffe auf Tripolis Libyen Verletzte
Majeruhi wakiwa hospitali, baada ya kushambuliwa na ndege za NATOPicha: AP

Hapo awali, shirika la habari la Libya -JANA- lilisema kuwa maeneo yanayokaliwa na raia katika mkoa wa Al-Qariet ulioko kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, yamekuwa yakilengwa na mashambulio hayo ya anga.