NATO kuondoka Libya karibuni. | Matukio ya Kisiasa | DW | 22.10.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

NATO kuondoka Libya karibuni.

Jumuiya ya NATO yakaribia kumaliza operesheni za kijeshi nchini Libya.

Jumuiya ya kijeshi ya NATO imesema itamazimaliza shughuli za kijeshi zilizoanza miezi saba iliyopita nchini Libya kufuatia kifo cha Kanali Muammar Gaddafi .

Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Anders Fogh Rasmussen amesema uamuzi huo bado ni wa muda na utatangazwa rasmi mapema wiki ijayo. Amesema anajivunia mafanikio yaliyofikiwa na NATO kwa kushirikiana na washirika wake katika harakati za kijeshi.

Wakati huo huo mzozo juu ya kanuni za kuushughulikia mwili wa Gaddafi umechelewesha maziko yake. Kwa mujibu wa kanuni za Kiislamu, mwislamu anapaswa kuzikwa haraka baada ya kufariki.

Lakini serikali ya Baraza la Mpito imesema mazingira yaliyosababisha kifo cha Gaddafi lazima yafanyiwe uchunguzi.

Hapo awali Waziri Mkuu wa serikali ya mpito alisema kuwa Kanali Gaddafi aliuawa wakati wa mapambano baina ya wafauasi wake na wapiganaji wa Baraza la Mpito.

Lakini picha za video zimefanya maswali yaulizwe.


 • Tarehe 22.10.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/12x1o
 • Tarehe 22.10.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/12x1o

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com