1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO iko tayari kufanya uchunguzi wa mauaji Libya

Sekione Kitojo20 Desemba 2011

Jumuiya ya NATO imesema leo kuwa ipo tayari kufanya uchunguzi juu ya madai ya vifo vya raia wakati wa kampeni ya mashambulizi ya anga nchini Libya iwapo itapata ombi hilo kutoka kwa viongozi wapya wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/13WGk
Vitaly Churkin, U.N. Russian Ambassador speaks at a Security Council meeting at U.N. headquarters Tuesday, Aug. 19, 2008 during emergency consultations on the conflict between Russia and Georgia after France requested discussion of a new draft plan to end the hostilities. (AP Photo/David Karp)
Balozi wa Urusi katika umoja wa mataifa Vitali Churkin ambaye sasa ni rais wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.Picha: AP

Hayo yamejiri baada ya balozi wa Urusi katika umoja wa mataifa Vitaly Churkin kusema kuwa atalipeleka suala hilo katika baraza la usalama la umoja wa mataifa wiki hii baada ya makadirio yaliyochapishwa katika jarida la New York Times kusema kuwa mashambulio ya NATO yamesababisha vifo vya kati ya watu 40 hadi 70 nchini Libya.

Akijibu madai hayo , msemaji wa jumuiya ya NATO Oana Lungescu , amesema kuwa ujumbe wa jumuiya hiyo nchini Libya umeokoa maisha ya watu kadha. Ameongeza kuwa mashambulio ya NATO yalichukua kila aina ya tahadhari kupunguza uwezekano wa vifo kwa raia.

Ameongeza kuwa NATO inachukulia madai hayo kwa dhati., na kwamba inaangalia ushahidi uliopo kwa makini.

Balozi wa Urusi katika umoja wa mataifa Vitaly Churkin amesema kuwa amekuwa akiiomba NATO kutoa ripoti kamili katika baraza la usalama la umoja wa mataifa inayotoa muhtasari wa shughuli zake nchini Libya. Lakini amesema kuwa kwa bahati mbaya jumuiya hiyo imetoa tu , ripoti ya juu juu tu, ambayo haikuwa na taarifa za kutosha.

Danish air force F-16 fighter planes maneuver as they prepare for landing at the Nato airbase in Sigonella, Italy, Saturday, March 19, 2011. NATO's top decision-making body is meeting in emergency session Saturday to review military plans for a no-fly zone over Libya. The North Atlantic Council is expected to issue the order to launch the operation during this weekend. Officials said the military staff was putting the final touches on plans to deploy dozens of fighter-bombers, tankers, helicopters and surveillance planes to several air bases along Europe's southern rim. (AP Photo/Andrew Medichini)
Ndege za kijeshi za NATO zikiruka katika anga ya LibyaPicha: AP

Urusi ni rais wa baraza hilo la usalama mwezi huu na Churkin amewaambia waandishi habari kuwa atalifikisha suala hilo kuuwawa kwa raia katika baraza la usalama la umoja wa mataifa wakati baraza hilo litakapokuwa linaijadili Libya siku ya Alhamis.

Kampeni ya anga ya NATO iliyodumu miezi saba dhidi ya Libya ilipigiwa upatu kuwa ni ushindi wa jumuiya hiyo pamoja na waungaji wake mkono kwa kuweka nchi hiyo katika njia sahihi kuelekea katika hatua ya mpito ya demokrasia baada ya kuondolewa madarakani na kuuwawa kwa dikteta Moammar Gaddafi.

Mark Kornlbau , msemaji wa ujumbe wa Marekani katika umoja wa mataifa , amesema kuwa kampeni ya NATO ililengwa katika kuwalinda raia wa Libya.

Lakini wakosoaji wa kampeni hiyo , ikiwa ni pamoja na Urusi, China na umoja wa Afrika , wamedai kuwa NATO ilitumia vibaya azimio la umoja wa mataifa lililoweka hatua ya ndege za Libya kutoruka katika anga la nchi hiyo na kuamuru ulinzi wa raia kama kisingizio cha kuhamasisha mabadiliko ya utawala nchini Libya.

Kwa bahati mbaya ,NATO ilielemea katika mfumo wa propaganda halisi, ikidai kuwa hakuna raia aliyeuwawa nchini Libya , hali ambayo ilikuwa si sahihi , Churkin amesema.

Men chant slogans during a protest in Benghazi, Libya, Monday, Dec. 12, 2011. Arabic writing on the banner, right, reads "Libyan youth will protect the revolution, Feb. 15" (Foto: Ibrahim Alaguri/AP/dapd)
Waandanaji vijana wakiandamana nchini Libya.Picha: dapd

Wakati huo huo huko Libya kwenye kumefanyika maandamano dhidi ya baraza la taifa la mpito, huku waandamanaji wakidai uhuru wa kutoa maoni na kwamba walioutumikia utawala wa Gaddafi kwa kuwa wapambe wake wa karibu wasiruhusiwe kushika nyadhifa muhimu za taifa hivi sasa. Wanadai mapinduzi mapya. Maandanamo hayo yameanzia tena katika mji wa pwani wa Benghazi, kiini cha vuguvuru la upinzani lililosababisha Gaddafi kuangushwa.

Mwandishi: Sekione Kitojo(afp

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman.