1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nani kusimamia ujenzi gaza ?

3 Machi 2009

Hamas au Mahmud Abbas ?

https://p.dw.com/p/H4ZG
Hillary Clinton(w.wa nje)Picha: AP

Kwa muujibu wa hesabu zilizofanywa na wapalestina , kuujenga upya mwambao wa Gaza , kutagharimu si chini ya Euro bilioni 2.2.Hivyo ni kusema, kiasi cha Euro bilioni 3 unusu-kima kikubwa zaidi kuliko ilivyotazamiwa. Mkutano wa Kimataifa Wafadhili, umeahidi kuchangia fedha hizo. Kikao cha Sharm El Sheikh,nchini Misri,swali hasa halikuwa tu kuchanga fedha,bali pia mustakbala wa Mashariki ya Kati.

Waziri mpya wa mammbo ya nje wa Marekani bibi Hilary Clinton aliewasili leo Israel,alibainika jana kuweka matumaini makuu.Alisema huko Sharm el Sheikh,Misri, mtu hawezi kuvumilia tena misukosuko zaidi na kuchelewesha mambo zaidi.Mchango wa Marekani katika kuijenga upya Gaza ,aliueleza Bibi Clinton kuwa sehemu ya mkakati wa siasa ya nje ya Marekani katika "safu mbali mbali" kupalilia amani ya kweli kati ya Israel na majirani zake wa kiarabu.

Wajum,be wengine mkutanoni huko Sharm el Sheikh,hawakuonesha staha ya kidiplomasia walipodhirisha kosa katika a msingi wa mkutano huu wa Mashariki ya Kati: Kosa lenyewe ni kuwa, "bila ya Israel kufungua mipaka ya kuingilia Gaza, juhudi zote zinazofanywa hazitafanikiwa".Hazitafaulu kuwapa matumaini wapalestina milioni 1.5 kuwa wiki 6 baada ya kumalizika mashambulio ya kijeshi ya Israel, kuwa nyumba na maskani zao yalioteketezwa ,majengo ya serikali yataweza kujengwa upya mnamo muda mfupi ujao.

Ni kuifungua mipaka hiyo ndiko hasa alikokataa waziri-mkuu wa Israel anaeacha madaraka Ehud Olmert.Anashikilia kwamba, kwanza yule mwanajeshi wa Israel Gilad Shalit,alietekwa na wapiganaji wa hamas 2006 aachwe huru.Ama sihivyo, kila kitu kitabakia kama kilivyo sasa......

Mrithi anaetazamiwa sana kukkalia kiti cha Bw.Olmert, Benjamin Netanyahu hatii sana maanani kuifungua mipaka ya kuingilia Gaza.Hivi sasa kuna mapatano ya wasi wasi ya kusimamisha vita huko Gaza.Waziri mkuu Olmert alitia munda siku chache tu kabla ya mkutano wa wafadhili wa Sharm el Sheikh juhudi za waziri wake wa ulinzi Ehud Barak na kati kati ya upatanishi wa Misri, kukubaliana kusimamisha kabisa vita na adui yake.Anadai kwamba haiwezekani kuafikiana na chama hiki cha Hamas.

Msimamo sawa na huo kuelekea chama cha Hamas unafuatwa tangu na waziri mpya wa mambo ya nje wa Marekani hata na umoja wa Ulaya.

Kwahivyo, fedha za kuijenga upya Gaza ,inakusudiwa kumiminwa mfukoni mwa mwenyekiti wa chama cha PLO,Mahmud Abbas amabe wadhifa wake wa Urais wa Mamlaka ya Ndani ya Wapalestina ulimalizika muda wake miezi 2 iliopita na Mamlaka yake ya ndani hayana sauti huko Gaza.

Kwa hali ilivyo, mara tu wajumbe wa Mamlaka ya ndani wakianza kutumia fedha hizo kuujenga upya mwambao wa gaza,kutazuka patashika mpya baina ya wapalestina wenyewe kwa wenyewe.Kwani, mnamo miezi 20 iliopita,Hamas imechukua jukumu mikononi mwake la kutawala pekee Gaza na kusarifu binafsi matumizi ya fedha na misaada.

Endapo alivyobashiri waziri wa nje wa Uingereza, Miliband kuwa msaada huu mpya ulioidhinishwa hautaweza kutumika huko Gaza,hapo tena tutarudi katika mtindo ule ule wa kujenga na kubomoa.