1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAJAF: Watu wengine 22 wauwawa

29 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWe

Watu wengine 22 wameuwawa leo kwenye mashambulio mbalimbali nchini Irak huku Washia wakiadhimisha maombolezi ya Ashura.

Hapo awali polisi walisema vikosi vya usalama vya Irak na Marekani viliwaua wapiganaji 300 karibu na mji mtakatifu wa Najaf.

Mapigano yameendelea leo kati ya wanajeshi wa Irak wakisaidiwa na wanajeshi wa Marekani dhidi ya wanamgambo wa kundi lisilojulikana tangu mapigano yalipozuka hapo jana kaskazini mwa Najaf.

Imeripotiwa wanajeshi watatu wa Irak wameuwawa katika mapigano hayo. Jeshi la Marekani limesema wanajeshi wawili waliuwawa wakati helikopta yao ilipotunguliwa.

Gavana wa eneo hilo amesema wanamgambo hao walipania kuwashambulia mashehe wa kishia hii leo huku mahujaji wakiendelea kukusanyika kwa maombolezi ya Ashura.