1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Wanawake 700 waandamana kudai nafasi zaidi bungeni

15 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYs

Mamia ya wanawake nchini Kenya wameandamana hii leo ili kudai kupewa nafasi zaidi bungeni katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka.Yapata wanawake 700 kutoka mikoa yote minane ya Kenya wamewakilisha ombi lililotiwa saini alfu 1 la kudai nafasi 50 bungeni.Hilo linaweza kutekelezwa endapo kipengee maalum cha katiba kinafanyiwa marekebisho.Bunge la Kenya lina nafasi 222 ambapo wanawake kwa sasa wanachukua nafasi 18.

Kulingana na utafiti idadi hiyo ya wabunge wanawake inaiweka Kenya kwenye nafasi ya 111 sawa na mataifa ya Sao Tome na Principe kati ya mataifa 136 kote ulimwenguni.Rwanda inaongoza ulimwenguni huku takriban nusu ya wabunge wake wote ni wanawake.