1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Waislamu watisha kuandamana kupinga unyanyasaji

31 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBU3

Waislamu nchini Kenya wanasisitiza kuandamana ili kupinga kuzuiliwa bila hatia,kurejeshwa nchi nyingine bila sababu za msingi,mateso aidha unyanyasaji.Siku moja baada ya kuandamana hadi makao makuu ya polisi wanaharakati hao walifanya mkutano wa hadhara katika msikiti mkubwa kabisa mjini Nairobi na kushikilia kuwa wanaendelea na maandamano.

Polisi waliwakamata baadhi ya watu kwenye mpaka wa Kenya na Somalia katika miezi ya Januari na Februari baada ya majeshi ya Ethiopia yakishirikiana na jeshi la Somalia kuwafurusha wapiganaji wa mahakama za kiislamu mjini Mogadishu.

Kundi la kutetea haki za binadamu la Rights Forum waliwasilisha ombi rasmi linalotaka raia 18 wa Kenya waliokuwa baadhi ya kundi la watu 150 waliopelekwa Somalia,Ethiopia na Guantanamo Bay.Kulingana na kundi hilo walikamatwa bila kutolewa mashtaka na baadhi yao kuteswa.

Waislamu nchini Kenya wanailamu serikali kwa kuyumbishwa na Marekani inayosema kuwa wapiganaji wa mahakam za kiislamu wanatumiwa kama maficho ya kundi la kigaidi la Al Qaeda.Kundi hilo linalaumiwa kwa kutekeleza mashambulio ya mabomu katika balozi zake za Kenya na Tanzania mwaka 98.

Serikali ya Kenya kwa upande wake haijasema lolote kuhusu maandamano hayo mpaka sasa.