Nairobi.Polisi wavunja vibanda kitongoji cha Mathare. | Habari za Ulimwengu | DW | 07.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Nairobi.Polisi wavunja vibanda kitongoji cha Mathare.

Polisi wa Kenya wameingia katika kitongoji kimoja mjini Nairobi leo , wakifyatua risasi na kuvunja vibanda wanavyoishi watu katika siku ya tatu ya msako dhidi ya ngome kuu ya kundi la wahalifu la Mungiki linalosadikiwa kuwa limefanya wimbi la mauaji.

Mamia ya polisi pamoja na wanajeshi wakiwa na silaha pamoja na marungu walilivamia eneo la Mathare, wakivunja vibanda vya mabati, wakiwapiga watu na kuwakamata wanaume, wanawake na watoto.

Milio ya bunduki imekuwa iksikika kila mara , amesema mwandishi mmoja wa shirika la habari la reuters. Watu kadha walilazwa kifudifudi ardhini, mikono yao ikiwa imefungwa nyuma.

Kundi la Mungiki lilianzishwa katika miaka ya 90 kama madhehebu ya dini lakini polisi wanasema kuwa ni moja kati ya makundi ya kihalifu kama kundi la Mafia nchini Itali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com