1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi.Kundi la waasi kusini mwa Ethiopia lazitaka nchi za Afrika kuishawishi nchi yao.

10 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuA

Kundi jengine la waasi linalopigania taifa huru kusini mwa Ethiopia limesema kuwa, linataka mataifa mengine ya Afrika yawasaidie na kuishawishi serikali ya Ethiopia ishiriki katika mazungumzo ya amani huko Addis Ababa.

Chama cha ukombozi wa Oromo (OLF) kimesema, kimezitaka Kenya, Nigeria na Afrika ya Kusini kwa ajili ya kulipatanisha kundi hilo na serikali ya Ethiopia ili kumaliza miongo ya mizozo katika jimbo hilo tajiri kwa rasilimali.

Mkuu wa masuala ya nje wa chama cha OLF Fido Abba akizungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP mjini Nairobi amesema kuwa kundi hilo linahitaji huruma kuto kwa watu wa Afrika.

Aidha ameongeza kuwa kwa miaka kadhaa sasa amekuwa akishangazwa na ukimwa wa nchi za Afrika juu suala la mzozo wao.