1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Dawa ya Ukimwi yapigwa marufuku

10 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaR

Serikali ya Kenya inatangaza kuwa inasitisha matumizi ya dawa ya kupunguza makali ya Ukimwi iliyoagizwa kurudishwa barani Ulaya.Dawa hiyo ilipatikana kuwa imeathiriwa.

Dawa hiyo kwa jina Nelfinavir iliagizwa kurejeshwa barani Ulaya mwezi Juni baada ya kampuni ya kutengeza dawa ya Uswisi ya Roche Holding AG kupata kemikali isiyokubaliwa katika dawa hizo.

Takriban wakenya 600 walikuwa wanatumia dawa hiyo baada ya kupewa katika vituo vya afya vya serikali.Kwa sasa wagonjwa hao wanatumia dawa aina ya Kaletra iliyo na nguvu kama za dawa iliyopigwa marufuku kulinga na Mkuu wa Huduma za Afya Dr James Nyikal.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali yapata watu milioni 1.3 wana virusi vya Ukimwi nchini Kenya huku viwango vya maambukizi mapya vikipungua kutoka asilimia 14 hadi 6.9.Takriban wakenya laki moja 20 wanatumia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi ARV.