Nairobi. Waliomshambulia Ngugi wahukumiwa kifo. | Habari za Ulimwengu | DW | 16.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Nairobi. Waliomshambulia Ngugi wahukumiwa kifo.

Walinzi watatu wamehukumiwa kifo jana kwa kumshambulia muandishi wa vitabu wa Kenya na mkewe wakati watu hao walipoitembelea Kenya kwa mara ya kwanza baada ya miaka 22 ya kuishi uhamishoni. Ngugi wa Thiong’o na mkewe walifanyiwa unyama na kuporwa mali mwaka 2004 baada ya walinzi kuvunja nyumba waliyokuwa wakiishi katika mji mkuu wa Kenya Nairobi. Watu hao walikuwa wafanyakazi wa jengo alimokuwa akiishi Wathiong’o.

Mawakili wa walinzi hao Richard Kayago Maeta, Elias Shikuku Wanjala na Peter Mulati Wafula amesema kuwa watakata rufaa. Thiong’o ambaye ni mkosoaji mkubwa wa utawala wa kikoloni, ukristo pamoja na hali mbaya baada ya ukolini , aliondoka nchini Kenya na kwenda kuishi mjini London na baadaye New York katika miaka ya mwanzo ya 1980 baada ya kuwekwa jela mwaka mmoja bila ya kufikishwa mahakamani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com