1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi: Wakaazi wa Kibera wapata nyumba mpya

17 Septemba 2009

Takriban familia 1000 za mtaa wa mabanda wa kibera jijini Nairobi zitanufaika na mpango wa kuboresha mitaa ya mabanda nchini Kenya uliozinduliwa leo katika mtaa huo wa Kibera.

https://p.dw.com/p/JiGb
Eneo la Kibera, jijini NairobiPicha: DW

Mpango huo ulioanzishwa mwaka 2004 na Serikali ya Kenya kwa Ushirikiano na Shirika la Makazi la Umoja wa mataifa UN Habitat umeanza kutekelezwa leo kwenye sherehe ya uzinduzi iliyoongozwa na Waziri Mkuu Raila Odinga. Jumla ya majengo 17 ya ghorofa tano kila moja yenye nyumba 600 za vyumba vitatu ziko tayari kwa wakazi kuingia. Kutoka Nairobi Mwandishi wetu Alfred Kiti ametutumia taarifa ifuatayo…