Nairobi. Viongozi wa Afrika wajadili kuhusu hali katika eneo la maziwa makuu. | Habari za Ulimwengu | DW | 15.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Nairobi. Viongozi wa Afrika wajadili kuhusu hali katika eneo la maziwa makuu.

Viongozi wa Afrika jana wamesifu hatua za maendeleo kuelekea amani katika eneo tete la maziwa makuu katika bara hilo , lakini wakatoa wito wa kuchukuliwa hatua za kuweza kuimarisha hali ya uimara, usalama na maendeleo. Viongozi hao wanaohudhuria mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu eneo la maziwa makuu, ambao umefunguliwa siku ya Jumatatu, wamekubaliana kuwa hatua zaidi zinahitajika kuliweka eneo hilo katika njia ya ukuaji wa uchumi na kuzuwia kuzuka tena kwa machafuko.

Eneo la maziwa makuu limekumbwa na vita vibaya sana duniani, katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan amesema katika ujumbe uliosomwa na mshauri wake maalum kwa bara la Afrika Joseph Legwaila.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com