NAIROBI: Ubalozi wa Marekani waonya juu ya hofu ya kufanywa shambulio | Habari za Ulimwengu | DW | 06.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI: Ubalozi wa Marekani waonya juu ya hofu ya kufanywa shambulio

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umesema umetahadharishwa juu ya uwezekano wa shambulio la kigaidi dhidi ya mashindano ya kimataifa ya mbio za nyika yatakayofanyika nchini Kenya mwishoni mwa mwezi huu.

Ubalozi huo umetoa taarifa inayosema tisho hilo linatoka kwa baadhi ya watu wenye msimamo mkali wa kidini. Taarifa hiyo pia imesema ubalozi wa Marekani unajua kuhusu matamshi yaliyotolewa hadharani na viongozi wa kiislamu katika mkoa wa pwani wakitishia kuvuruga mashindano hayo kwa njia ambazo hawakuzitaja, kama serikali ya Kenya haitatimiza masharti yao. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.

Mashindano ya kimataifa ya mbio za nyika yamepangwa kufanyika tarehe 24 mwezi huu mjini Mombasa, Kenya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com