1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Makasisi wa Marekani watawazwa uaskofu

30 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUN

Askofu mkuu wa Kianglikana nchini Kenya Benjamin Nzimbi amewatawaza makasisi wawili wakihafidhina wa Marekani kuwa maaskofu leo hii kuungoza waaumini wa Marekani ambao wamejitenga na kanisa la Kianglikana kutokana na msimamo wake juu ya suala la mashoga.

William Atwood na William Murdoch ni miongoni mwa idadi inayoongezeka ya makasisi wa Marekani wanaoahidi utiifu kwa maaskofu wa Afrika ambao wana msimamo mkali dhidi ya mashoga na ndoa za jinsia moja.

Atwood na Murdoch watasimamia makundi 30 ya waumini nchini Marekani ambayo yametaka uongozi kutoka Kenya.