1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Kongamano la kimataifa lamalizika

26 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXv
"Tatizo ni ubaguzi wa kimbari"
"Tatizo ni ubaguzi wa kimbari"Picha: picture-alliance/ dpa

Mkutano wa kimataifa juu ya masuala ya kijamii, „World Social Forum“ umemalizika katika mji mkuu wa Kenya,Nairobi.Mkutano huo wa siku sita umesifiwa na wanaharakati wanaotumia nafasi ya mkutano huo kujadili masuala muhimu yanayohusika na nchi za Kiafrika kama vile vita dhidi ya UKIMWI,njaa na umasikini.Katika sherehe za kuufunga mkutano huo,mshindi wa zawadi ya amani ya Nobel,Wangari Maathai alitoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kufuta madeni ya nchi za Kiafrika zilizo masikini sana.