1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Homa ya bonde la ufa yaua 30.

30 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfA

Zaidi ya watu 30 wamefariki kutokana na homa inayojulikana kama homa ya bonde la ufa kaskazini ya Kenya katika muda wa wiki moja iliyopita. Ugonjwa huo unaombukizwa kupitia virusi, ambao unadalili kama za mafua unaambukizwa kutoka mifugo kwenda kwa binadamu kupitia mbu.

Ugonjwa huo umekuwa hatari zaidi kutokana na mafuriko katika eneo hilo.

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu linasambaza vyandarua kwa watu katika eneo hilo ili kusaidia kuzuwia ugonjwa huo kuweza kusambaa zaidi.

Tangu mwezi wa Oktoba zaidi ya watu 150 wamefariki kutokana na mafuriko pamoja na magonjwa yanayoambatana na hali hiyo baada ya mvua ambazo si za kawaida kunyesha nchini humo.