1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Bunge lashutumiwa na tume ya rushwa

14 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPy

Tume ya kupiga vita rushwa nchini Kenya hapo jana imeshutumu bunge kwa kukwamisha hatua za serikali kuiruhusu tume hiyo kuchunguza uhalifu uliotendeka kabla ya mwezi wa Mei mwaka 2003.

Mkuu wa tume hiyo Aaron Ringers amesema kile ilichokifanya bunge itaifanya Kenya ionekane kuwa kichekesho mbele ya jumuiya ya kimataifa ambapo watu wengine hawatoona kazi yao kuwa ni ya makini.

Amesema kwa hatua hiyo wamekuwa wamewapa msaada na faraja wala rushwa.

Wabunge hapo Jumaatano wameyakata mapendekezo ya serikali kwa sheria ambayo itawapa madaraka tume ya rushwa kuchunguza madai kabla ya kutumika kwa sheria hiyo hapo mwezi wa Mei mwaka 2003.

Sheria ya sasa inaizuwiya tume hiyo kuchunguza kupotea kwa mamia ya mamilioni ya dola kwa kupitia miradi ya rushwa chini ya tawala za Rais wa zamani Daniel arap Moi ambaye amestaafu hapo mwaka 2002 na aliechukuwa nafasi yake Mwai Kibaki.