1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : 450 wauwawa katika muda wa miezi mitano

5 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79l

Zaidi ya vijana 450 wa Kenya wameuwawa katika mtindo wa mauaji ya magenge katika kipindi cha miezi mitano iliopita.

Repoti iliotolewa na Tume ya Taifa ya Haki za Binaadamu nchini Kenya leo hii imeyahusisha mauaji hayo na vita kati ya polisi na kundi la kikatili la kikabila linalotuhumiwa kuchinja watu kadhaa na kuwapiga risasi kulikopelekea maafa mapema mwaka huu.

Repoti ya tume hiyo ya haki za binaadamu ya serikali imesita kuwalaumu polisi moja kwa moja kwa mauaji hayo lakini imesema ushahidi wa kimazingira unaihusisha na vifo vingi dai ambalo polisi inalikanusha vikali.