1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Naibu Kamishna wa Polisi akamatwa kwa mashambulizi Ethiopia

Bruce Amani
25 Juni 2018

Idadi ya waliokufa kutokana na shambulizi la guruneti kwenye mkutano wa hadhara katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, imefikia watu wawili.

https://p.dw.com/p/30ECk
Äthiopien Premierminister Abiy Ahmed in Addis Ababa | Demonstration mit Anhängern
Picha: Reuters

Watu 30 wamekamatwa kuhusiana na mlipuko huo wakiwemo polisi kadhaa, akiwemo naibu kamishna wa polisi wa Addis Ababa.

Shambulizi hilo lilitokea katika uwanja mkubwa wa wazi uliokuwa umefurika, wakati Waziri Mkuu Abiy Ahmed akikamilisha hotuba yake mbele ya maelfu ya watu siku ya Jumamosi.

Vurugu zilizozuka baada ya mripuko huo wakati watu walianza kukimbilia jukwaani ziliwajeruhi watu 150.

Hakuna aliyetangaza kuhusika na shambulizi hilo lisilo la kawaida katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, ambao kila mara huwa na ulinzi mkali.

Ethiopia imesema kuwa Marekani itawatuma wapelelezi wa FBI ili kusaidia kuchunguza shambulizi hilo.