NAHR EL- BARED : Wanamgambo wagoma kusalimu amri | Habari za Ulimwengu | DW | 03.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAHR EL- BARED : Wanamgambo wagoma kusalimu amri

Wanajeshi wa Lebanon wameshambulia maeneo ya wanamgambo wa kundi la Kipalestina la Fatah al Islam kutaka kuwatokomeza kutoka kwenye kambi ya wakimbizi wa Kipalestina walikojichimbia lakini kundi hilo limeapa kwamba katu halitosalimu amri.

Abu Salim Taha msemaji wa kundi hilo amesema hakuna njia itakayowafanya wasalimu amri kwa kuwa hiyo ni fahari yao.

Wanajeshi hao wa Lebanon wameshambulia kwa makombora na mizinga na kuteketeza kabisa majengo mawili ya ghorofa refu na kuyaacha mengine kadhaa yakifuka moshi.

Wanajeshi watano wameuwawa tokea kuanza kwa mashambulizi mapya hapo Ijumaa.

Mapambano hayo ya siku 13 kati ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo hao yameuwa zaidi ya watu 100 wengi wao wakiwa ni raia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com