1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NABLUS:Hali ya kawaida yarudi ukingo wa magharibi

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCO2

Israel imewaondoa wanajeshi wake katika mji wa Nablus katika ukingo wa magharibi.

Hatua hii imekuja baada ya opresheni ya siku tatu dhidi ya wanamgambo wa kipalestina iliyoendeshwa na wanajeshi hao.

Wanajeshi hao wameondoa amri ya kutotoka nje ambayo ilisababisha maeneo mengi ya kibiashara kufungwa ikiwa ni pamoja na shule lakini sasa kila kitu kimerudi katika hali ya kawaida.

Hata hivyo Israel haijathibitisha iwapo msako huo dhidi ya wanamgambo wa Kipalestina umemalizika.

Israel imesema ilianzisha opresheni hiyo kwasababu washambuliaji wengi wakujitoa muhanga katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wamekuwa wakitokea mjini Nablus.