1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NABLUS: Wapalestina watatu wauwawa na wanajeshi wa Israel

Wapalestina watatu wameuwawa leo kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel katika mapigano yaliyotokea kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.

Kwenye kambi ya wakimbizi ya Al Faraa, Saadi Subuh, mwenye umri wa miaka 23 na Mustafa Abu Zalat wa miaka 17 walipigwa risasi na kuuwawa wakati wanajeshi wa Israel walipowafyatulia risasi wapalestina waliokuwa wakiyalenga kwa mawe magari ya jeshi.

Msemaji wa jeshi la Israel amesema wapalestina wawili walikuwa na bunduki na shoka.

Katika kijiji cha Yamoun, Ahmed Abul Hassan wa umri wa miaka 28 alipigwa risasi kichwani na kuuwawa alipokuwa juu ya paa la nyumba yake akitazama uvamizi wa jeshi la Israel.

Lakini baadaye kundi la wanamgambo la Islamic Jihad limetoa taarifa katika Ukanda wa Gaza kwamba Hassan ni mwanachama wake aliyeuwawa katika mapigano makali na wanajeshi wa Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com