1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa Uturuki na mataifa ya Ulaya

15 Machi 2017

Reutlinger-General Anzeiger limejikita katika  uchaguzi wa  Uholanzi unaofanyika leo(15.03.2017) kwa mtazamo wa mvutano uliopo kati ya nchi hiyo na  Uturuki.

https://p.dw.com/p/2ZCX4
Türkei Erdogan Rede im Bestepe Zentrum in Ankara
Rais Recep Tayyip Erdogan wa UturukiPicha: picture-alliance/abaca/AA/M. Ali Ozcan

Mhariri anasema kwamba Chaguo bado lingali wazi, kwa sababu wengi miongoni mwa Waholanzi bado hawajaamua. Kitu kimoja kingali wazi nacho ni kwamba vyama  vinavyounda serikali ya mseto vitapoteza kura. Lakini pamoja na hayo vyama hivyo vitahakikisha chama  cha siasa kali za  kizalendo za mrengo wa kulia  kinashindwa. Sababu ni kwamba  Rais  Erdogan wa Uturuki ni mfano mmoja mzuri wa kile kinachoweza kutokea pindi  wenye siasa kali za kizalendo wanaingia madarakani.

Gazeti la Westfälische Nachrichten: Mhariri ameandika hivi,Nani anayetaka  vitisho, matusi na kufananishwa na Wanazi  na wakati huo huo  ajadiliane na Uturuki ? Huu sio tu  ni mzozo wa kidiplomasia, lakini huenda Uturuki ikajikuta ikitengwa kisiasa kwa muda mrefu. Mazungumzo na Umoja wa Ulaya kwa wakati huu hayana tija.

Kujiondoa kwenye mihimili ya kidemokrasi na ukiukaji wa Haki za binaadamu, kunaifungia njia Uturuki ya kuelekea Ulaya ilio huru na yenye amani."

Hannoversche Allgemeine Zeitung llimeandika juu ya  mabishano kati ya Scotland na serikali kuu ya Uingereza inayoongozwa na Theresa May kuhusu mpango wa kujitoa katika Umoja wa  Ulaya:

Uingereza inatarajiwa kuanza mchakato wa kujitoa rasmi katika Umoja wa Ulaya. Jee Uhuru wa Scotland inayopinga mpango huo ndiyo  Suluhisho.  Huenda kukawa na nafasi chungu nzima pindi hilo likitokea, lakini pia  kuna  athari  nyingi mpya .  Kutokana na hayo wanaopinga Uingereza kujitoa  katika Umoja wa Ulaya  wamekuwa wakati wote wakionya kwamba Itakuwa zawadi kubwa kwa Waingereza  kusema Kwaheri Umoja wa ulaya , kwani kwa huenda ikwa ni tija kwa Scotland- tija ya kutaka kujitenga.

Neue Osnabrücker Zeitung limezingatia uamuzi wa Mahakama kuu ya Ulaya  kwamba waajiri wanaweza kupiga marufuku uvaaji wa vazi la hijabu makazini:

Uamuzi wa mahakama kuu ya Ulaya ni wakusisimua kwa sababu ni kuhusu haki za msingi. Dini ni jambo la binafsi na hata  waajiri wamelazimika kukubaliana nalo. Kuna  tafauti kati ya uhuru wa  kuabudu na haki za kibiashara. Uamuzi huo wa mahakama kuu ya Ulaya  unafafanua kwamba  uhuru wa kuabudu katika jamii ya  mchanganyiko wa watu wa dini tafauti hauna mipaka. Sasa ni juu ya mwajiri mwenyewe kuamua ,anapiga marufuku au la. Na hiyo ni ishara  kamili ya kuwepo kwa  uhuru na kuvumiliana.."

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman/ Dt Zeitungen
Mhariri:Yusuf Saumu