1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo kuhusu timu ya Ufaransa wazua mjadala wa kitaifa

21 Juni 2010

Rais Sarkozy asema lazima wachezaji wawajibike.

https://p.dw.com/p/Nyai
Nikolas Anelka aliyefukuzwa kutoka katika timu ya Ufaransa.Picha: AP

Mzozo ndani ya timu ya taiafa ya Ufaransa katika kombe la dunia unaendelaea kugonaga vichwa vya habari baada ya mshambuliaji Nicolas Anelka kukorofishani na Kocha wake na kurudishwa nyumbani.Mshauri wa rais Nikolas Sarkozy wa Ufaransa katika mahojiano na gazeti la Le Parisien, amesema kwamba rais huyo anataka timu ya Ufaransa iwajibike kutokana na matukio ya kususia mazoezi baada ya kufukuzwa kwa mchezaji Nikolas Anelka. Vyombo vya habari nchini Ufaransa vimelipa kipa umbele suala hilo vikisema ni matukio yalioleta aibu kubwa kwa taifa zima.

Mshauri wa rais wa Ufaransa alisema rais Sarkozy anataka uchunguzi ufanywe na timu ya Ufaransa ya kandanda iwajibike. Haya yanajiri wakati taifa zima bado linakumbwa na mshtuko hasa baada ya wachezaji wa timu ya Ufaransa katika michuano ya kombe la dunia inayoendelea Afrika kusini,kususia mazoezi wakipinga kufukuzwa kwa mchezaji mshambuliaji Nikolas Anelka anayetuhumiwa kwa kumtusi kocha Raymond Domenech.

Televisheni nchini Ufaransa bado zinaendelea kuonyesha picha ya majibizano kati ya nahodha wa timu ya Ufaransa, Patrice Evra na mkufunzi wa viungo, Robert Duverne baada ya wachezaji kukataa kufanya mazoezi.

Na huku timu hiyo ikiwa imesalia na mechi moja dhidi ya Afrika kusini hapo kesho, nafasi ya kufuzu kwa duru ya pili ni finyu sana. Waziri wa michezo wa Ufaransa Roselyn Bachelot katika mahojiano na televisheni ya TF1 alisema rais Sarkozy alimtaka asalie Afrika kusini ili ajaribu kurejesha hali ya utulivu.

Waziri Bachelot alisema alipanga mkutano wa dharura na Evra, Domenech na mkuu wa shirikisho la kandanda la Ufransa, Jean- Pierre Escalettes na akaomba pande zote ziwajibike na ziwe na nidhamu. Wakati huo huo ghadhabu dhidi ya mienendo ya wachezaji wa Ufaransa imekuwa suala la kitaifa nchini Ufaransa na waziri wa mambo ya nchi za nje Bernard Kouchner amesema tabia ya wachezaji hao inaidhalilisha Ufaransa na ni sinema ya aibu.

Gazeti la Le Parisien limesema kwamba timu hiyo imewaaibisha na kwenye ukurasa wa mbele wa gazetu hilo ni kichwa, uasi ikiwa juu ya picha ya wachezaji wa timu hiyo. Gazeti hilo limesema kwamba wachezaji hao walikuwa kama watoto watukutu waliofanya walichotaka kutokana na shinikizo za wakubwa wao bila ya kuwajibika kabla ya mechi inayosubiriwa dhidi ya Afrika kusini.

NO FLASH Frankreich Streik WM 2010
Wachezaji wa timu ya Ufaransa walisusia mazoezi baada ya kufukuzwa kwa Anelka.Picha: AP

Mchezaji Nikolas Anelka alikasirika na kujibizana na kocha wake wakati wa kipindi cha mapumziko. Ufaransa ilishindwa na Mexico kwa mabao 2 kwa bila na lazima iishinde Afrika kusini kwa mabao mengi ili ijiongezee nafasi ya kuingia katika duru ya pili ya michuano.

Mchezaji wa zamani wa timu ya Ufaransa aliyeiwezesha timu hiyo kushinda kombe la dunia la mwaka 1998, Zinedine Zidane amesema hajafurahishwa na tabia ya wachezaji hao. Zidane amesema amesikitishwa na mazungumzo yaliyokuwa ya faragha kugeuka kuwa ya hadhara na kufichuliwa na vyombo vya habari. Zinedine Zidane amepinga kwamba alitoa mwelekeo kwa timu ya Ufaransa kabla ya kushindwa na Mexico mabao 2 kwa bila.

Mwandishi, Peter Moss, DPA/AP/AFP

Mhariri, Abdul-Rahman Mohammed