1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MZIKI WA KALE HAKIKA UNA ULIMBO

Christopher Buke21 Mei 2007

Hata vijana wananaswa na mziki wa aina hii

https://p.dw.com/p/CHcA

“Weka Remmy Ongala!” alihanikiza kijana mmoja aliyekuwa katika baa iitwayo Masiwa Family mjini Bagamoyo ambapo kwa nasibu siku hiyo nilitoka ili kujumuika na rafiki zangu ili kutoa ushamba machoni.

Kijana huyu alitoa ombi lake mara mbili na akiisha gundua kuwa DJ kampuuza na kuweka wimbo mwingine aliinamisha kichwa chake na kuendelea ‘kupata taratibu’, kama wafanyavyo waungwana.

Badala ya kumsikiliza mteja yule DJ aliweka wimbo ambao nadhani aidha aliutaka au aliodhani unapendwa zaidi na wateja wengi. Wimbo huo ni wa 20 % uitwao Binti kimanzi. Basi ndo ukatutumbuiza si unajua tena mara “ ukitaka utamuoa eeh mtoto tulia”, na kadhalika na kadhalika.

Baadhi ya niliokuwa nao wakaonyesha hisia za kuvutiwa na wimbo huo. Mwenzangu yule aliyekuwa ameomba wimbo wa Dk. Remmy ambaye alikuwa amekaa meza ya katikati ya ukumbi wa baa ile akaendelea kuinamsiha kichwa chake. Binafsi nikadhani amekubali matokeo, kumbe bado analo.

Mara tu wimbo huo wa 20 % ulipokuwa unaishiria akapaza tena sauti yake “Tuwekee Remmy Bwana”, bahati mbaya na mara hii hakusikilizwa. Mbaya zaidi hata wimbo uliowekwa na DJ safari hii na sisi ukaanza kutuboa.

Taarabu yenyewe ikawa si taarabu maana inaimba kwa kuzorota kama vile kanda ina matatizo. Mwenzangu yule akaendelea kuinamisha kichwa mara hii akilaani kichini chini.

Mara moja nikajifunza kitu na hivyo nikawauliza rafiki zangu tuliokuwa tumekaa meza moja kama wanaweza kugundua kwa nini yule jamaa hatulii bila kuchezewa wimbo wa Dk. Remmy Ongala?

Mwenzangu mmoja aliyeonekana kuwa shapu kujibu swali langu alimwangalia kwa udadisi kisha akanijibu “ halafu jamaa mwenyewe anaonekana kachoka!”, kikafuata kicheko tena cha kuiba-iba, si unajua mambo ya baa? ili isibainike tunacheka nini.

Lakini baada ya kicheko na mimi kama paparazzi nikadadisi na kisha nikakubaliana na mada iliyokuwa imetolewa na mwenzangu namimi. Nadhani huenda ikawa ndio sababu ya kutaka achezewe mwimbo wa Remmy Ongala.

Na kusema kweli hili ndo likaja kunikumbusha maneno aliyowahi kuniambia Dk. Remmy ongala Mwenyewe pale nilipomuuliza sababu ya nyimbo zake nyingi kuzungumzia zaidi mambo ya kawaida kabisa ambayo twakutana nayo katika maisha ya kila siku?

“ Nalikuwa natunga kwa sababu nalikuwa mi napenda sana wanyonge. Wale wa under dog. Watu wa masikini ndio nilikuwa napendelea sana kuzungumzia nyimbo zangu.

Sana nilikuwa napendelea kuzungumzia wamasikini kwa sababu mimi ni masikini pia, na masikini hakuna mtu wa k