1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwito kuunga mkono makubaliano ya kugawana madaraka Kenya

6 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DJt8

NAIROBI:

Rais wa Kenya Mwai Kibaki ametoa mwito kwa bunge kuidhinisha makubaliano ya kugawana madaraka yaliyomaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.Kufuatana na makubaliano hayo,kutazinduliwa wadhifa wa waziri mkuu;na vyama vya Rais Kibaki na kiongozi wa upinzani Raila Odinga alie waziri mkuu mteule vitagawana nyadhifa katika baraza la mawaziri.

Makubaliano hayo yalipatikana juma lililopita baada ya kufanywa majadiliano marefu chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan.Zaidi ya watu 1,000 waliuawa na maelfu wengine wamepoteza makaazi yao katika machafuko yaliyozuka kufuatia uchaguzi wa Desemba 27 uliombakisha madarakani Rais Kibaki.