Mwandishi habari wa Ufaransa auawa Syria | Matukio ya Kisiasa | DW | 12.01.2012
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mwandishi habari wa Ufaransa auawa Syria

Ufaransa inaitaka Syria kuanza kuchunguza mauaji ya ripota wa Kifaransa yaliyotokea katika mji wa Homs nchini Syria.

This is an undated photo provided Wednesday Jan.11, 2012 by France 2 television shows French television reporter Gilles Jacquier, at an unknown location who has been killed Wednesday Jan 11, 2012 in unknown circumstances in Homs, Syria. France 2 says Jacquier, was on an Syrian government-authorized reporting trip to the Arab country at the time of his death. Another member of the reporting team was uninjured. (Foto:AP/dapd) NO SALES

Mwandishi habari Gilles Jacquier ameuawa Homs,Syria

Katika taarifa iliyotolewa mjini Paris, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Alain Juppe vile vile amelaani kile alichokiita kitendo kinachokirihisha. Gilles Jacquier ni mwandishi habari wa kwanza wa nchi ya magharibi kuuawa nchini Syria, tangu maandamano dhidi ya Rais wa Syria Bashar al-Assad kuanza miezi 10 iliyopita.

Mwandishi habari huyo wa Kifaransa, ni miongoni mwa watu 8 waliouawa hapo jana, baada ya kujikuta katikati ya mapambano wakati wa kutembelea eneo hilo, baada ya kupata kibali cha serikali, ambalo ni jambo la nadra. Mwandishi habari wa Kiholanzi pia, ni miongoni mwa watu 25 waliojeruhiwa katika shambulio hilo. Syria imewapiga marufuku waandishi habari wengi wa kigeni tangu machafuko kuibuka nchini humo hapo mwezi Machi.

 • Tarehe 12.01.2012
 • Mwandishi Martin,Prema/zpr
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13hxl
 • Tarehe 12.01.2012
 • Mwandishi Martin,Prema/zpr
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13hxl

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com